1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PARIS: Rais Obasanjo kiongozi wa AU akitaja kitendo cha Kumba Yalla kuwa jaribio la mapinduzi

26 Mei 2005
https://p.dw.com/p/CF9s

Kiongozi wa Umoja wa Afrika, Rais wa Nigeria Oleshegun Obasanjo amekitaja kitendo cha rais wa Gueinea Bissau aliyeondolewa madarakani bwana Kumba Yalla kuwa jaribio la mapinduzi.

Obasanjo ameyasema hayo akiwa kwenye ziara yake ya siku nne nchini Ufaransa.

Obasanjo ametaka uchaguzi wa nchi hiyo ufanyike kama ulivyopangwa kufanyika tarehe 19 mwezi juni.

Bwana Kumba Yalla aliyeondolewa madarakani mwezi septemba mwaka2003 lakini akajitangaza May 15 kwamba bado ni rais wa Gueine Bissau,aliivamia na kuiteka ofisi ya rais kwa takriban muda wa saa nne mapema hapo jana huku akiwa na wanajeshi na kuzusha hali ya wasiwasi nchini humo.

Licha ya Kumba Yalla kupigwa marufuku ya kujihusisha katika siasa kwa kipindi cha miaka mitano,Mahakama kuu nchini humo mapema mwezi huu ilimruhusu kushiriki katika kinyanganyiro cha kuwania urais katika uchaguzi ujao.