1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Pazia la Bundesliga lafunguliwa

9 Agosti 2013

Kocha wa mabingwa wa Bundesliga Bayern Munich, Pep Guardiola amesisitiza kuwa yuko tayari kukikabili kikosi cha kocha Lucien Favre cha Moenchengladbach leo jioni(09.08.2013)katika mpambano wa ufunguzi wa Bundesliga.

https://p.dw.com/p/19N6d
ARCHIv - Die Mannschaft des Fußball-Bundesligsiten FC Bayern jubelt am 11.05.2013 nach dem Spiel FC Bayern München gegen FC Augsburg mit Meisterschale. Der FC Bayern ist Deutscher Meister der Saison 2012/13. Foto: Tobias Hase/dpa (zu dpa-Meldung: «Trainer und Manager sicher: Bayern München wieder Meisterfavorit» vom 05.08.2013) +++(c) dpa - Bildfunk+++
FC Bayern MünchenPicha: picture-alliance/dpa

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 42 ambaye ni kocha wa zamani wa Barcelona amekuwa na wiki chini ya nane tu kuifunza Bayern , ambayo itatiana kifuani jioni ya leo dhidi ya Moenchengladbach katika uwanja wa Allianz Arena mjini Munich.

Bayern haitapata huduma ya mchezaji aliyesajiliwa hivi karibuni Thiago Alcantara wakati nahodha huyo wa timu ya taifa ya Uhispania ya vijana chini ya miaka 21alishindwa kufanya mazowezi jana Alhamis kwa kuwa alikuwa na homa. Guardiola tayari ameonesha kile ambacho anakiweza akiwa Bayern , akianzisha mfumo mpya wa mchezo na kujaribu kuwahamisha wachezaji kutoka katika nafasi zao za kawaida.

Lucien Favre, head coach of Borussia Moenchengladbach reacts during the Champions League Qualification soccer match against Dynamo Kiev at the Olympiyskiy national stadium in Kiev, Ukraine, Wednesday, Aug. 29, 2012. (Foto:Efrem Lukatsky/AP/dapd).
Lucien Favre wa GladbachPicha: dapd

Baada ya kuongoza michezo 11 ya kabla ya msimu , pamoja na kipigo cha mabao 4-2 dhidi ya Borussia Dortmund katika mchezo wa Super Cup wiki mbili zilizopita ikiwa ni kipigo pekee, Guardiola ana ushauri muhimu kwa wachezaji wake.

"Chezeni mpira, jisikieni raha na shambulieni mnavyoweza", amesema katika mkutano wake na waandishi wa habari kabla ya mpambano huu wa leo.

Fußball Testspiele Uli Hoeneß Cup FC Bayern München - FC Barcelona am 24.07.2013 in der Allianz Arena in München (Bayern). Pep Guardiola, Trainer von München gestikuliert am Spielfeldrand. Foto: Marc Müller/dpa pixel
Pep Guardiola wa Bayern MunichPicha: picture-alliance/dpa

Bayern Munich iliikandika Borussia Moenchengladbach kwa mabao 5-1 katika muda wa dakika 60 za mchezo wa fainali ya Telecom Cup wiki tatu zilizopita, lakini Guardiola amesisitiza kuwa anatarajia mchezo hatari kutoka kwa Gladbach, kwa kuwa wana kocha mwerevu sana.

Ni moja kati ya timu bora kabisa katika Bundesliga, na ni lazima tusahau ushindi wetu wa hivi karibuni, ameongeza Guardiola.

MOENCHENGLADBACH, GERMANY - MAY 03: (L-R) Julian Draxler of Schalke celebrates the first goal wioth Raffael during the Bundesliga match between Borussia Moenchengladbach and FC Schalke 04 at Borussia Park Stadium on May 3, 2013 in Moenchengladbach, Germany. (Photo by Christof Koepsel/Bongarts/Getty Images)
Wachezaji wa Schalke 04 ambao watapambana na Metalist Kharkiv ya UkrainePicha: Getty Images

Doping haina nafasi katika Bundesliga

Wakati huo huo shirikisho la soka la Ujerumani DFB pamoja na shirika la kupambana na wanamichezo wanaotumia madawa ya kuongezea nguvu misuli NADA, wamethibitisha kuwapo mkataba mpya ambao utahusisha udhibiti wa zaidi ya hatua 500 za udhibiti katika msimu huu wa 2013 na 2014 wa Bundesliga, ikiwa ni pamoja na uchunguzi wa damu katika michezo nchini Ujerumani .

Michuano ya mtoano Champions League

Nayo michezo ya mtoano ya Champions League imepangwa leo ambapo Schalke 04 ya Ujerumani itapambana na Metalist Kharkiv ya Ukraine, timu ambayo inakabiliwa na uchunguzi wa shirikisho la kandanda barani Ulaya , UEFA kutokana na madai ya kupanga matokeo.

Kesi hiyo itakayofanyika Jumanne ijayo itaamua iwapo timu hiyo ya Ukraine inastahili kushiriki katika michezo hiyo ya mtoano ama la. Celtic ya Scotland itapambana na Shakhtar Karagandy pia ya Kazakhstan, na Arsenal London ina miadi na Fenerbahce ya Uturuki, wakati AC Milan mabingwa mara saba wa Champions League inakwaana na PSV Eindhoven.

Mwandishi : Sekione Kitojo / afpe / dpae

Mhariri: Gakuba Daniel