PEKING: Njia za reli zitakuwa za kisasa Nigeria
2 Novemba 2006Matangazo
Nigeria na China zimetia saini mkataba wa kupanua njia za reli na kuzifanya za kisasa katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi.Kwa mujibu wa vyombo vya habari,mradi huo utagharimu Dola bilioni 8.3 na unatazamia kujenga njia ya reli kati ya mji mkuu wa biashara wa Nigeria Lagos na Kano.Njia hiyo itakayokuwa na urefu wa kilomita 1,300 inatarajiwa kuwa tayari katika muda wa miaka mitano.