PEKING:Umoja wa Mataifa unaomba michango kwa ajili ya Korea Kaskazini ili ...
20 Novemba 2003Matangazo
kuepusha njaa katika nchi hiyo ya kikoministi. Mkurugenzi wa Mpango wa Chakula wa Umoja wa Mataifa katika Korea Kaskazini, Rick Corsino, amearifu mjini Peking, kuwa mwaka ujao zinahitajiwa dollar zaidi ya millioni 220 kwa ajili ya msaada wa chakula na madawa. Corsino alisisitiza, Korea Kaskazini inaendelea kutegemea mno msaada zaidi wa kiutu. Utapiamlo umefikia kiwango cha kustua mno katika nchi hiyo.