Pingamizi dhidi ya Musharraf kugombea tena urais zaendekea,Pakistan
4 Oktoba 2007Wapinzani hao wawili wa Musharraf katika uchaguzi huo wa urais wanasema kuwa kama mkuu wa majeshi hastahili kugombea urais. Malalamishi mengine ni kuwa kura hiyo ya kumachagua rais haipaswi kupigwa na wabunge walioko sasa ambao muhula wao unamalizika mapema mwaka ujao.
Matamshi hayo yanawadia baada ya kiongozi wa jopo la majaji 10 wanaosikiliza kesi hiyo Javed Iqbal kuuliza iwapo kuharishwa kwa uchaguzi huo wa urais ni kwa manufaa ya wapakistan. Hamid Khan ,wakili wa Wajihuddin Ahmad alijibu swali hilo kwa kusema kuwa kutatoa machafuko iwapo uchaguzi huo utafanyika na nikutokana na kuepruka hali hiyo tunapendekeza uchaguzi huo uhairishwe.
Ahmad, ambaye alikuwa jaji katika mahakama kuu, ni mmoja wa wagombea urais katika uchaguzi huo wa siku ya jumamosi. Mwingine ni naibu mwenyekiti wa chama cha upinzani, Pakistan Peoples Party cha Benazir Bhutto.
Katika kile kinachoonekana kama pigo kubwa kwa upinzani wiki iliyopita mahakama kuu nchini Pakistan ilimruhusu Musharraf kubakia mkuu wa majeshi na vilevile kukitetea kiti cha urais.Baadaye tume ya uchaguzi nchini humo ilipuuzilia mbali malalamishi yao dhidi ya ugombezi wa Musharraf.
Mawakili wa serikali walisema kwa kuhairisha uchaguzi huo kutaifanya Pakistan ambaye ni rafiki mkubwa marekani kuchekwa na ulimwengu. Uhusiano kati ya rais Musharraf na mahakama kuu umekuwa si mzuri, tangu alipojaribu kumfuta kazi jaji mkuu iftikhar Muhammad Chaudry mwezi marchi.
Musharrf kutoka taifa pekee lka kiislamu linalounda silaha za kinuklia anatarajiwa kushinda katika uchaguzi huo siku ya jumamosi.Musharraf wa umri wa miaka 64 ameahidi punde baada ya kuchaguliwa rais atangatuka madarakani kama mkuu wa majeshi tarehe 15 mwezi ujao.
Tarrifa nyingine ni kuwa aliyekuwa waziri mkuu wa pakistan Benazir Bhutto amesema anatajia kupewa msamaha na Rais Musharraf kuhusiana na mashtaka ya ufisadi. Katika mashauri ambayo yamekuwa yakiendelea kwa miezi kadhaa kati ya Bhutto, Musharraf kuhusu kugawana mamlaka , swala hilo limekuwa miongoni mwa yale yanajadiliwa kwa kina.
Msemaji wa Bi Bhutto Wajid Hasan aliliambia shirika La habari la kimataifa la AFP bado wanasubiri kielelezo cha maridhiano kutoka kwa afisi ya rais Musharraf kinachotarajiwa kutumwa leo. Matamshi hayo yanawadia wakati ambapo serikali ya rais Musharraf imeleza kufanikiwa kwa mashauri kati yao na Bi bhutto, hali inayoashiria kuwa huenda tangazo la msamaha dhidi ya Bhutto likatolewa wakati wowote.
Bi Bhutto ambaye ameahidi kurejea nyumbani tarehe 18 mwezi huu amekuwa uhamishoni tangu mwaka 1999.
Bhutto ambaye alikuwa waziri mkuu kati ya mwaka 1988 na 1990 na tena mwaka 1993 na 1996 anapinga hatua ya musharraf kugombea urais akiwa bado mkuu wa majeshi.