Pizzaro kujadili na Bayern kuhusu kazi ya ubalozi
11 Julai 2020"Siku zote nilisema nilipata ofa ya kupendeza kufanya kitu kwa Bayern," Pizarro aliuambia mkutano wa waandishi wa habari Jumatano (08.07.2020). "Sasa ni wakati wa kufikiria kuhusu hilo. Ni lazima pia kuangalia na kuoa ni kipi kilicho bora kwa familia yangu."
Mwenyekiti wa klabu ya Bayern Munich Karl-Heinz Rummenigge mnamo mwaka jana alisema kuwa Pizarro mwenye umri wa miaka 41 anaonekana kufaa kuwa balozi wa klabu ya Bayern.
Pizarro aliichezea Bayern mnamo mwaka 2001 hadi 2007 na tena mwaka 2012 hadi mwaka 2015 huku akishinda mataji mengi likiwemo taji la ligi ya mabingwa wa ligi ya Ulaya, Champions, ligi kuu ya kandanda ya Ujerumani, Bundesliga, na kombe la shirikisho la Ujerumani, DFB Pokal.
Alicheza jumla ya mechi 490 za Bundesliga wakati akisakata kandanda katika klabu ya Bremen, Bayern na FC Cologne na kupachika kimiani magoli 197.
Huku akiikodolea macho kazi ya ubalozi mjini Munich, Pizzaro alisema mechi ya kuaga lazima ichezwe Bremen ambako alianza maisha yake ya kusakata kabumbumbu nchini Ujerumani mnamo 1998 na kukamilisha safari yake Jumatatu 06.07.2020.
"Bila shaka mechi itachezwa uwanja wa Weser Stadium," Pizzaro alisema, akiongeza kwamba hakuna tarehe iliyopangwa kwa sababu ya janga la virusi vya corona.
(dpa)