1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Poland kujiimarisha kijeshi kutokana na hofu ya uvamizi

22 Septemba 2023

Waziri Mkuu wa Poland Mateusz Morawiecki amesema nchi yake haiipi tena Ukraine silaha, kwa sababu nchi hiyo inajiimarisha yenyewe kijeshi kutokana na hofu ya uvamizi wa Urusi katika kanda hiyo.

https://p.dw.com/p/4Wgfr
Poland, Waziri Mkuu Mateusz Morawiecki
Waziri Mkuu wa Poland Mateusz MorawieckiPicha: Damian Burzykowski/IMAGO

Waziri Mkuu wa Poland Mateusz Morawiecki amesema nchi yake haiipi tena Ukraine silaha, kwa sababu nchi hiyo inajiimarisha yenyewe kijeshi kutokana na hofu ya uvamizi wa Urusi katika kanda hiyo.

Hayo yanajiri mnamo wakati mzozo wa kibiashara kati ya mataifa hayo jirani yakiongezeka. Na chama chake cha siasa za kizalendo kikikabiliwa na shinikizo kutoka chama cha siasa kali za mrengo wa kulia kuelekea uchaguzi ujao wa kitaifa oktoba 15.

Chama cha mrengo wa kulia kimesema Poland haipati shukrani inayostahili kwa kuipa Ukraine silaha na kuwapokea wakimbizi wake.

Hisia zimekuwa zikiongezeka tangu Poland, Hungary na Slovakiazilipotangaza marufuku mpya dhidi ya uagizaji wa nafaka za Ukraine wiki iliyopita, wakisema walitaka kuwalinda wakulima wao.

Kwingineko rais wa Marekani Joe Biden ametoa ahadi ya kuipa Ukraine mifumo mipya ya ulinzi wa anga. Amesema hayo alipokutana na rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky anayefanya ziara nchini Marekani.