1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaPoland

Poland kuongeza wanajeshi kuwasaidiana walinzi wa mpakani

10 Agosti 2023

Poland inapanga kuongeza wanajeshi hadi 1,000 kwenye mpaka wake na Belarus, watakaosaidiana na walinzi wa mpakani.

https://p.dw.com/p/4V0so
Polen | Verlegung von Truppen an die polnisch-belarussische Grenze
Wanajeshi wa PolandPicha: 12 Brygada Zmechanizowana/Handout/REUTERS

Waziri wa ulinzi wa Poland Mariusz Blaszczak, amesema hii leo kwamba karibu wanajeshi 1,000 wataongezwa mpakani, na miongoni mwao, 4,000 watasaidiana moja kwa moja na Walinzi wa Mpakani na wengine 6,000 watakuwa wa ziada.

Blaszczak amesema wanapeleka jeshi karibu na mpaka na Belarus ili kuwatisha wavamizi na kuwazuia wasijaribu kuwashambulia.

Poland imekuwa na wasiwasi zaidi na eneo hilo mpaka tangu baada ya mamia ya mamluki wa kundi binafsi la kijeshi la Urusi la Wagner, walipokwenda Belarus mwezi uliopita kwa mwaliko wa Rais Alexander Lukashenko.