1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Poland yatoa usafiri wa bure kwa watu wanaokwenda Ujerumani

10 Machi 2022

Kampuni ya reli ya Poland PKP imetangaza leo Alhamisi itatoa tiketi za bure kwa raia wa Ukraine wanaosafiri kuelekea sehemu mbalimbali za Ujerumani.

https://p.dw.com/p/48JKB
Finnland | Menschen aus St. Petersburg am Bahnhof in Helsinki
Picha: Antti Aimo-Koivisto/Lehtikuva/dpa/picture alliance

Kufikia jana Jumatano, raia wa Ukraine waliruhusiwa kusafiri bure kwenye treni tisa za kila siku za kati zinazounganisha miji ya Poland ya Warsaw, Przemysl kupitia Krakow na Gdynia hadi mji mkuu wa Ujerumani, Berlin na mji wa mpakani wa Frankfurt. Tangu Urusi ilipoivamia Ukraine mnamo Februari 24 na kuongezeka kwa wimbi kubwa la wakimbizi nchini Poland, kampuni ya reli ya Poland imeongeza treni zaidi kutoka mpaka wa Ukraine na kuruhusu watu wanaokimbia nchini kuzitumia bila malipo. Naibu Waziri wa Mambo ya Nje Pawel Szefernaker ameiambia leo televisheni ya taifa kwamba wakimbizi wengi walikuwa wakipiga kambi katika vituo vya treni vya Poland, wakitarajia kusafiri kwenda nchi nyingine za Umoja wa Ulaya.