Polisi Afrika Kusini yasubiri uamuzi wa kumkamata Zuma
6 Julai 2021Wiki iliyopita, mahakama ya katiba nchini humo ilimhukumu Zuma kifungo cha miezi 15 jela, kwa hatia ya kukaidi agizo la mahakama na ilimtaka ajisalimishe polisi kabla ya Jumapili kumalizika na ikiwa hatafanya hivyo basi polisi wapewe muda wa siku tatu kumtia nguvuni.
Waziri wa idara ya polisi nchini Afrika Kusini Bekhi Cele, amesema anasubiri uamuzi wa mahakama, ikiwa rais huyo wa zamani akamatwe au la baada ya kukaidi agizo la mahakama la kumtaka ajisalimishe.
soma zaidi: Zuma apuuza agizo la kujisalimisha kwa polisi
Zuma mwenye umri wa miaka 79 pia aliwasilisha rufaa nyingine tofauti katika mahakama ya katiba kubatilisha uamuzi wa kutaka afungwe. Rufaa hiyo itasikilizwa Julai 12.
Zuma anakabiliwa na tuhuma za kuhusika na ufisadi katika kipindi cha utawala wake uliodumu wa miaka tisa.