1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Polisi Kenya kufanya uchunguzi wa mauaji ya watu waliotupwa

13 Julai 2024

Jeshi la Polisi nchini Kenya limesema linachunguza iwapo kuna polisi waliohusika katika ugunduzi wa kutisha wa miili iliyokatwakatwa na kutupwa kwenye sehemu ya taka mjini Nairobi.

https://p.dw.com/p/4iFbS
Japhet Koome
Japhet Koome amejiuzulu katika nafasi ya Mkuu wa polisi wa kitaifa kufuatia maandamano nchini KenyaPicha: AP Photo/picture alliance

Jeshi la Polisi nchini Kenya limesema linachunguza iwapo kuna polisi waliohusika katika ugunduzi wa kutisha wa miili iliyokatwakatwa na kutupwa kwenye sehemu ya taka mjini Nairobi.

Mamlaka Huru ya Kusimamia Polisi (IPOA) pia inachunguza madai ya kutekwa nyara na kukamatwa kinyume cha sheria kwa waandamanaji walitoweka baada ya maandamano makubwa ya kuipinga serikali.

Soma zaidi. Miili sita ya wanawake waliokatwa yakutwa dampo Nairobi

Vikosi vya usalama vya Kenya viko chini ya uangalizi kuhusu vifo vya watu kadhaa wakati wa maandamano mwezi uliopita. Jeshi hilo linatuhumiwa na makundi ya kutetea haki za binadamu kwa kutumia nguvu kupita kiasi.

Siku ya Ijumaa, Mkuu wa polisi wa kitaifa Japhet Koome, mlengwa wa hasira nyingi ya umma kutokana na vifo vya waandamanaji, alijiuzulu katika nafasi hiyo baada ya chini ya miaka miwili katika wadhifa huo.