1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Polisi nchini Tanzania yawakamata viongozi wa upinzani

23 Septemba 2024

Polisi nchini Tanzania imewakamata viongozi wawili wa upinzani leo, wakilenga kuzima maandamano ya umma yaliyoandaliwa kwenye mji wa kibiashara nchini humo wa Dar es Salaam.

https://p.dw.com/p/4kyIJ
Tanzania I Freeman Mbowe - Kiongozi wa upinzani, Chadema
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA amekamatwa baada ya kujaribu kuongoza maandamano ya kupinga utekaji na mauaji nchini TanzaniaPicha: Michael Jameson/AFP/Getty Images

Taarifa zilizotolewa na polisi pamoja na makao makuu ya chama kikuu cha upinzani nchini humo cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA zinasema waliokamatwa ni Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe na Makamu wake Tundu Lissu.

Duru zinaeleza kwamba Mbowe alikamatwa kwenye eneo la Magomeni maili chache kutoka katikati ya mji. Alikuwa akijiandaa kuongoza maandamano ya wafuasiw wa CHADEMA ya kulaani visa vya utekaji nyara na mauaji ya wanachama wake.

Chama cha Demokrasia na Maendeleo kinaituhumu serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan kuirejesha nchi hiyo ya Afrika Mashariki kwenye utawala kandamizi sawa na wa mtangulizi wake, John Magufuli.