Polisi Uhispania yamsaka aliyekuwa kiongozi wa Catalonia
8 Agosti 2024Kiongozi huyo anayepigania uhuru wa Catalonia alirejea leo nchini Uhispania na kisha akatoweka tena katika hali isiyoeleweka baada ya kutoa hotuba mjini humo.
Inadaiwa kuwa alisaidiwa kukwepa mtego kwa msaada wa polisi mmoja wa eneo hilo ambaye ametiwa mbaroni.
Aliwahutubia mapema leo maelfu ya wafuasi wake katikati ya Barcelona mbele ya maafisa wa polisi ambao hawakufanya jaribio lolote la kumkamata.
Baada ya hotuba aliondoka haraka akitumia gari lililokuwa likimsubiri. Matukio hayo yalijiri karibu miaka saba baada ya Puigdemont kukimbia Uhispania baada ya jaribio lililoshindwa la uhuru, na kukatolewa waranti wa kukamatwa kwake.
Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 61, awali alitangaza nia yake ya kuwa nchini Uhispania katika siku ambayo bunge la Catalonia lilitarajiwa kumuapisha rais mpya.
Puigdemont mwanzoni aliishi Ubelgiji baada ya kukimbia Uhamisho mwaka wa 2017, lakini mahali anakoishi kwa sasa hapajulikani.