1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Polisi Uingereza katika hali ya tahadhari

9 Agosti 2024

Serikali ya Uingereza imesema inajiandaa kwa uwezekano wa kutokea machafuko zaidi licha ya kupongeza juhudi za polisi na wanaharakati wa kupinga ubaguzi wa rangi kuzuia ghasia zaidi.

https://p.dw.com/p/4jIPv
Großbritannien Demonstration gegen Einwanderungsproteste
Picha: Burak Bir/Anadolu/picture alliance

Waziri Mkuu Keir Starmer ametoa tahadhari hiyo kufuatia wiki ya machafuko yaliyochochewa na habari za upotoshaji kuhusu mauaji ya wasichana watatu.

Starmer aliongoza mkutano mwengine wa dharura na mawaziri waandamizi na viongozi wa polisi jana Alhamisi ili kujiweka tayari kwa uwezekano wa kutokea machafuko.

Mkuu wa polisi Gavin Stephens ameeleza kuwa, kuna watu wenye nia ya kufanya vurugu na uharibifu lakini polisi wako macho.

Takriban watu 500 wamekamatwa nchini Uingereza baada ya makundi ya watu wenye kupinga uhamiaji na Uislamu kukabiliana na polisi na kushambulia misikiti na hoteli wanamolala waomba hifadhi.