1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Ugaidi

Polisi Ujerumani yatoa vidio ya mshukiwa wa kundi la RAF

12 Septemba 2024

Polisi Ujerumani imetoa video mpya na picha za mwanamume wanayemshuku kuwa mwanachama wa kundi maarufu zaidi - Kikundi cha Jeshi Nyekundu au RAF - ambacho kiliitikisa Ujerumani Magharibi katika miaka ya 1970 na 80.

https://p.dw.com/p/4kWwR
Washukiwa wa Rwaf wanaosakwa na pilisi Garweg na Staub
Washukiwa wa Rwaf wanaosakwa na pilisi Garweg na StaubPicha: Julian Stratenschulte/dpa/picture alliance

Wanachama wanaosakwa kwa muda mrefu wa kundi la mrengo mkali wa kushoto la Red Army Faction, RAF, ambalo lilikuwa kitisho cha ugaidi kwa Ujerumani kwa miongo kadhaa, hivi sasa wanaaminika kushiriki matukio kadhaa zaidi ya ujambazi, kulingana na waemdesha mashta.

Vidio mpya, picha na taarifa kuhusu magaidi wa zamani Burkhard Garweg na Ernst-Volker Staub, inatumika kuwafuatilia washukiwa hao. Wanaume hao wanaaminika kufanya mashambulizi dhidi ya magari ya kusafirisha fedha taslimu na maduka makubwa, kati ya 1996 na 2016, wakiwa pamoja na Daniela Klette, aliekamatwa mjini Berlin mwanzoni mwa mwaka huu.

Watatu hao waanchunguzwa kwa makosa ya ujambazi mkubwa na jaribio la mauaji, pamoja na utekaji na utozaji pesa kwa nguvu. Shirika lao lililoua zaidi ya watu 30, lilitangaza kuvunjika mwaka 1998.