1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Polisi watumia mabomu ya machozi kutawanya waandamanaji DRC

20 Mei 2023

Vikosi vya usalama nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo vimetumia mabomu ya machozi kuwatawanya waandamanaji mjini Kinshasa kuipinga serikali kwa madai ya kuwepo kwa dosari katika uandikishaji wa wapiga kura.

https://p.dw.com/p/4Rc8n
Sehemu ya mji mkuu wa Kongo, Kinshasa
Sehemu ya mji mkuu wa Kongo, KinshasaPicha: Jane Barlow/PA Wire/empics/picture alliance

Waandamaji kadhaa walikamatwa na askari wa usalama mara baada ya kuanza kwa maandamano hayo yaliyoitishwa na viongozi wa upinzani.

Viongozi hao ni pamoja na Martin Fayulu aliyeshika nafasi ya pili katika uchaguzi wa mwaka 2018 pamoja na mfanyabiashara na gavana wa zamani, Moise Katumbi .

Mbali ya suala la uandikishaji wapiga kura, waandamanaji wamekasirishwa  na kupanda kwa gharama za maisha pamoja na ukosefu wa usalama wa muda mrefu katika eneo la mashariki mwa taifa hilo.

Waasi na makundi ya wabeba silaha wamekuwa wakifanya mashambulizi ambayo yamewauwa mamia ya watu kwenye eneo hilo na kusababisha wengine kuyakimbia makazi yao.