1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Polisi Kenya yawakamata wahalifu 270 kwenye maandamano

3 Julai 2024

Polisi ya Kenya inasema imewakamata zaidi ya watu 270 waliokuwa wanafanya vitendo vya kihalifu kwa kisingizio cha kushiriki maandamano ya kuipinga serikali hapo jana Jumanne.

https://p.dw.com/p/4hooL
Kenya | Maandamano Nairobi
Waandamanaji mjini Naorobi wapiga filimbi wakati wa maandamano ya kupinga mswada wa fedha.Picha: Monicah Mwangi/REUTERS

Haya yamesemwa na afisi ya Mkurugenzi wa Uchunguzi wa Jinai nchini humo katika ujumbe aliouandika kwenye mtandao wa X usiku wa kuamkia leo.

Inadaiwa kwamba jumla ya washukiwa 204 wa uhalifu wamekamatwa katika mji mkuu Nairobi na wengine 68 katika maeneo mengine nchini humo.

Soma pia: Hali nchini Kenya bado ni ya wasiwasi kufuatia maandamano

Vitendo vya uporaji na uharibifu mkubwa wa mali viliripotiwa wakati wa maandamano hayo yaliyoongozwa na vijana kote nchini humo, huku baadhi ya waandamanaji wakisema maandamano hayo yaliingiliwa na waporaji.

Maandamano ya Jumanne yalianza kwa amani ila yakageuka na kuwa machafuko huku polisi wakifyatua mabomu ya kutoa machozi nao waandamanaji wakiwarushia mawe mjini Nairobi.