Polisi yaapata kifaa inachoshuku kimetumika Solingen
24 Agosti 2024Taarifa hiyo inajiri baada ya ya watu watatu kuuwawa kwa kuchomwa visu siku ya Ijumaa katika tamasha lililokuwa mjini humo.
Watu Takriban wanane walijeruhiwa watano kati yao wanaripotiwa kuwa katika hali mbaya. Bado mshukiwa wa tukio hilo hajapatikana lakini polisi wamethibitisha kuendelea na uchunguzi wa kumtafuta aliyefanya kitendo hicho cha kinyama.
Hata hivyo ofisi ya mwendesha mashtaka mkuu imesema haijafuta uwezekano wa kuliita tukio hilo kuwa la kigaidi.
Scholz alaani shambulio la kisu lililowauwa watu watatu Solingen
Akizungumzia mkasa huo Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz amesema kuwa tukio la aina hiyo halikubaliki katika jamii na kwamba hatua kali za kisheria zinapaswa kuchukuliwa.
Scholz amelitaja shambulio hilo kuwa ni uhalifu wa kutisha na kwamba serikali itausaidia mji huo na watu wake kwa kila namna.