Polisi ya Uturuki yashutumiwa kutesa watu baada ya tetemeko
6 Aprili 2023Ripoti ya pamoja ya mashirika ya kutetea haki za binadamu imesema maafisa wa usalama wa Uturuki wamewatesa watu waliokamatwa kwa kushukiwa kwa uporaji baada ya tetemeko la ardhi lililoikumba nchi hiyo mnamo mwezi Februari.Tetemeko jipya la ardhi lazikumba Uturuki na Syria
Katika ripoti ya pamoja, mashirika ya Amnesty International na Human Rights Watch yamesema polisi ya Uturuki na jeshi walitumia hali ya tahadhari iliyotangazwa na Rais Recep Tayyip Erdogan baada ya tetemeko hilo la ardhi, kama ruhusa ya kuwatesa watu. Mashirika hayo yanasema wizara ya sheria ya nchi hiyo iilitoa jawabu kabla kutolewa kwa ripoti hiyo ikisema, Uturuki kamwe haikubali mateso ya watu ila wizara hiyo imeyapuuza yaliyomo katika ripoti hiyo. Ripoti hiyo inasema mtu mmoja alifariki mikononi mwa polisi baada ya kuteswa.