1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PORT-AU-PRINCE:Maafa ya vimbunga kwenye eneo la Atlantik

25 Oktoba 2005
https://p.dw.com/p/CEOn

Kimbunga Alpha kilichovuma kisiwani Haiti kimesababisha si chini ya vifo 10,wamearifu maafisa wanaoshughulika na maafa nchini humo.Mito imefurika na nyumba nyingi zimeteketezwa na kimbunga hicho.Kwa upande mwingine Kimbunga Wilma kilichotangulia kuvuma katika eneo la Atlantik, kimesababisha mvua kubwa katika jimbo la Florida nchini Marekani.Hadi hivi sasa vifo 5 vimeripotiwa katika eneo hilo la Florida ambako kiasi ya watu milioni sita hawana umeme.Kwa upande mwingine,wizara ya utalii nchini Mexico imekadiria kuwa Kimbunga Wilma kimesababisha hasara ya kama Dola milioni 800 nchini humo. Kimbunga Wilma kilichovuma na upepo wa kasi ya kilomita 175 kwa saa,hivi sasa kimeelekea katika bahari ya Atlantik.