1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PORT HARCOURT: Mjerumani atekwa nyara Nigeria

4 Agosti 2006
https://p.dw.com/p/CDP5

Mfanyakazi wa Kijerumani ametekwa nyara katika mji wa Port Harcourt kusini mwa Nigeria.Kwa mujibu wa polisi,vijana waliovaa sare za kijeshi na kubeba silaha walisimamisha gari ya mfanyakazi huyo wa kampuni la Bilfinger Berger katika barabara kuu na wakamchukua na kuondoka nae katika boti.Mara kwa mara wafanyakazi wa kigeni wa mashirika ya mafuta wametekwa nyara katika eneo hilo lenye utajiri wa mafuta kusini mwa Nigeria na waasi wanaotaka kuona utajiri huo ukiwanufaisha wakazi wa jimbo hilo la Niger Delta.Lakini kundi la wanamgambo wanaopigania uhuru wa jimbo hilo kusini mwa Nigeria limesema halikuhusika na utekaji nyara wa siku ya Alkhamisi.Nigeria ni mzalishaji mkubwa kabisa wa mafuta barani Afrika,lakini idadi kubwa ya wananchi hawakunufaika na utajiri huo.