1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PORT HARCOURT: Nigeria yaadhimisha miaka kumi tangu kuuwawa Ken Saro Wiwa

10 Novemba 2005
https://p.dw.com/p/CEJo

Nigeria imeadhimisha miaka kumi tangu kuuwawa kwa Ken Saro Wiwa, mwandishi mashuhuri aliyepigania kumaliza uchafuzi wa mazingira unaosababishwa na viwanda vya mafuta nchini Nigeria.

Mwandishi mashuhuri wa riwaya wa Nigeria, Wole Soyinka, amemsifu Saro Wiwa, muongo mmoja baada ya shujaa huyo kunyongwa pamoja na watu wengine tisa kwa kupatikana na makosa ya mauaji na mahakama ya kijeshi. Inasemekana madai hayo yalikuwa njama ya serikali iliyokuwa madarakani wakati huo.

Mwanasiasa wa eneo anakotoka Saro Wiwa, Lebum Micce, amewaambia waandamanaji 5,000 mjini Port Harcourt, kwamba mapambano yanaendelea na wanatakiwa kuendelea kumkumbuka shujaa wao.