PRAGUE. Jamhuri ya Ucheki yakabiliwa na mzozo wa kisiasa.
15 Aprili 2005Serikali ya jamhuri ya Ucheki kwa mara nyengIne tena inakabiliwa na mzozo wa kisiasa kufuatia kusarambatika kwa mkataba uliofikiwa na vyama vitatu vya kisiasa kuunda serikali mpya. Chama cha Social Democrats cha waziri mkuu Stanislav Gross, kiliukataa mpango huo, ambao ungemlazimu Gross kujiuzulu pasipo uchaguzi mwengine kuitishwa nchini humo. Chama hicho kinasema mpango huo uliwapendelea washiriki wake wa awali katika serikalini. Chama cha Christian Democrats kilijiondoa kutoka muungano huo kufuatia kashfa ya fedha iliyomkabili waziri huyo mkuu, hatua iliyoisababisha serikali kupoteza idadi kubwa ya wabunge. Makubaliano ya jana yangefutilia mbali uwezekano wa kufanyika uchaguzi wa mapema nchini humo, na kukiruhusu chama cha Social Democrats kuendelea kutawala kikiwa na idadi ndogo ya wabunge.