Prague. Polisi yazima maandamano.
11 Novemba 2007Polisi pamoja na waandamanaji wapatao 1,000 ambao walifanya ghasia wamezuwia maandamano ambayo yamepigwa marufuku yaliyokuwa yafanywe na kundi la Manazi mamboleo katika mji mkuu wa jamhuri ya Chek wa Prague.
Zaidi ya polisi 1,500 wenye silaha walifunga eneo linaloishi Wayahudi ambapo kiasi cha wanachama 400 wa kundi lenye msimamo mkali wa mrengo wa kulia walipanga kukutana kuadhimisha enzi za utawala wa Kinazi wa walipowakamata Wayahudi na kujulikana kama Kristallnaght pogrom dhidi ya Wayahudi. Baadhi ya watu wamejeruhiwa baada ya mapambano kuzuka baina ya Wanazi mamboleo na waandamanaji wanaopinga maandamano hayo. Kiasi cha watu 80 wamekamatwa, miongoni mwao ni watu 50 wenye imani kali kwa kuwa na silaha. Mabasi matatu yaliyokuwa yamewabeba Wanazi mamboleo kutoka Ujerumani yalionekana mpakani kabla ya kusindikizwa na polisi.