1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Prague. Rais wa jamhuri wa Czech asema hakuna haja tena ya kuidhinisha katiba ya Ulaya ya sasa.

5 Juni 2005
https://p.dw.com/p/CF6l

Rais wa jamhuri ya Czech Vaclav Klaus amesisitiza leo kuwa hakuna sababu ya kuendelea na uidhinishaji wa katiba ya sasa ya umoja wa Ulaya kufuatia kukataliwa na wapiga kura wa Ufaransa na Uholanzi.

Bwana Klaus amesema katika mahojiano na kituo cha televisheni cha Czech , kuwa inafahamika kwamba katiba hiyo lazima iidhinishwe na mataifa yote 25 wanachama.

Amesema kuwa hapo kabla watu walikuwa na wasi wasi kuwa Uingereza itaikataa katiba hiyo. Kwa kuwa sasa nchi mbili zimekwisha ikataa hakuna sababu na kuendelea kuidhinishwa na mataifa mengine. Badala yake amesema ni lazima kutafuta njia nyingine ya kuiandika katika hiyo ambayo haitaingilia katika sehemu ya maisha ya wananchi.

Lakini pamoja na yeye binafsi kuipinga katiba hiyo , Bwana Klaus amesema hatazuwia hatua yoyote itakayofanywa na serikali ya Czech kufanya kura ya maoni kuidhinisha waraka huo.