PRAGUE: Urusi haitoruhusiwa kuiamuru NATO
22 Mei 2007Matangazo
Rais Vaclav Klaus wa Jamhuri ya Czech na mwenzake wa Poland Lech Kaczynski,wamesisitiza kuwa wanaunga mkono mpango wa Marekani wa kutaka kuweka makombora ya kujikinga katika nchi hizo mbili za Ulaya.Klaus amesema,mradi huo wa ulinzi nchini Jamhuri ya Czech na Poland utaimarisha uhusiano kati ya nchi zinazohusika.Marekani imesema,licha ya Urusi kuhamakishwa na mpango huo,Moscow haitoruhusiwa kuliamuru shirika la kujihami la magharibi,NATO juu ya maslahi ya kitaifa kuhusu usalama.Baada ya kukutana karibu na mji wa Prague kwa majadiliano yasio rasmi,marais Klaus na Kaczynski walieleza pia wasiwasi wao kuhusika na mdahalo wa Katiba ya Umoja wa Ulaya.