1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Premier League yasubiri msimu mpya wa VAR

22 Julai 2019

Mashabiki wengi wanasubiri sana kuanza msimu mpya wa ligi kuu ya kandanda ya England. Lakini kitu ambacho pia kinasubiriwa kwa hamu ni kuanza kutumiwa mfumo wa video katika kusaidia maamuzi ya refarii – VAR.

https://p.dw.com/p/3MXlp
Champions League Manchester City - Tottenham Hotspur
Picha: picture-alliance/AP Photo/D. Thompson

Kaimu afisa mkuu mtendaji wa Premier League Richard Masters amesema bila shaka mfumo huo utasababisha utata katika ligi, ikiwa ni mara ya kwanza unatumika, lakimi dosari zozote zitarekebishwa katika siku za usoni.

VAR tayari inatumika katika ligi nyingine kubwa za Ulaya ikiwemo Bundesliga ya Ujeurmani na La Liga ya Uhispania, pamoja na FA na League Cup nchini England. Msimu mpya wa Premier League unang'oa nanga Agosti tisa.

Masters anasema mashabiki wanataka kuona makossa ya wazi yakitendewa haki. Lakini hawataki kuona kandanda la Premier League likisitishwa kila mara au kasi ya mchezo ikipungua.

Ni maoni ambayo kiongozi wa mradi wa VAR katika shirikisho la kandanda la Ujeurumani – DFB ameyaunga mkono. Jochen Drees ameliambia jarida la Kicker kuwa mashabiki na wachezaji hawapaswi kusubiri kwa muda mrefu kwa maamuzi kuchukuliwa na refarii msaidizi wa video katika mechi za Bundesliga.

Refarii huyo wa zamani hata hivyo haamini kuwa mashabiki hivi karibuni wataweza kutizama kwenye skrini kubwa za uwanjani, picha sawa na wanazotazama maafisa kwenye VAR