Uchaguzi wa Naibu Meya wa Dar es Salaam Tanzania umefanyika hapo jana, na Mussa Kafana wa chama cha Wananchi, CUF, ambacho ni miongoni mwa vyama vinavyounda UKAWA akishinda. Hata hivyo uchaguzi huo ulikumbwa na dosari baada ya baadhi ya wajumbe wa pande zinazokinzana kulumbana hadi kufikia hatua ya kuvutana mashati. Msikilize mchambuzi Marcos Albanie alipozungumza na mwandishi wetu Isack Gamba.