Putin afanya mazunguzo na kiongozi wa mpito wa Mali
10 Septemba 2023Ikulu ya Kremlin imesema mazungumzo hayo yaliyofanyika kwa njia ya simu kati ya wawili hao, yalijikita katika masuala mbalimbali yakiwemo mzozo wa Niger ambayo ni jirani wa Mali, pamoja na juhudi za kupambana na ugaidi.
Taarifa ya Kremlin imeeleza kuwa Putin na Goita wamekubaliana kuwa mgogoro wa Niger uliotokana na mapinduzi ya mwezi Julai, unaweza kutatuliwa kwa njia za kidiplomasia pekee.
Soma pia: Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergei Lavrov, afanya ziara nchini Mali
Jumuiya ya Kiuchumi ya Mataifa ya Afrika ya Magharibi, ECOWAS, iliwahi kutishia kuiingilia kati kijeshi nchi hiyo ili kumrejesha madarakani Rais Mohamed Bazoum aliyepinduliwa.
Viongozi wa kijeshi wa Mali waliyatahadharisha mataifa ya nje yasiivamie kijeshi Niger na pia watawala hao wamekuwa na uhusiano wa karibu na Urusi, ambayo ilipeleka Vikosi vya wapiganaji mamluki wa kampuni ya Wagner nchini humo.