Putin ataja shambulizi mjini Belgord kuwa 'tukio la kigaidi'
1 Januari 2024Akizungumza wakati wa mkutano na wanajeshi wake katika hospitali moja ya kijeshi mjini Moscow, Putin amesema lazima hatua ichukuliwe kutokana na mashambulizi hayo yaliyofanyika wakati wa Urusi ikiimarisha mashambulizi ya anga dhidi ya miji ya Kyiv na Kharkiv.
Putin amesema kuwa wanajeshi wake wataendelea kulenga ''shabaha muhimu za kijeshi nchini Ukraine." Hata hivyo, Urusi imekanusha shutuma za mataifa ya Magharibi na Ukraine kwamba inalenga miundombinu ya kiraia.
Soma pia:Urusi yadai kuzima mashambulizi ya Ukraine katika ardhi yake
Katika mazungumzo hayo yaliyogusia masuala mbali mbali, Putin amesema kuwa mkondo wa vita nchini Ukraine unageuka kwa manufaa yaUrusi na kwamba nchi hiyo inatumai kumaliza vita hivyo lakini kwa mujibu wa matakwa yake.