1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Putin azituhumu nchi za Magharibi kwa mashambulizi Urusi

6 Aprili 2023

Rais wa Urusi Vladimir Putin ameyatuhumu mashirika ya usalama ya nchi za Magharibi kwa kuisaidia Ukraine kufanya kile alichokiita "mashambulizi ya kigaidi" nchini Urusi.

https://p.dw.com/p/4PkzG
Rais wa Urusi Vladimir Putin mjini Moscow
Rais wa Urusi Vladimir Putin Picha: Gavriil Grigorov/SNA/IMAGO

Rais wa Urusi Vladimir Putin ameyatuhumu mashirika ya usalama ya nchi za Magharibi kwa kuisaidia Ukraine kufanya kile alichokiita "mashambulizi ya kigaidi" nchini Urusi. Putin ameyasema haya baada ya kuwapa makaribisho baridi mabalozi wa Marekani na Umoja wa Ulaya nchini humo.

Rais huyo wa Urusi alikuwa akizungumza katika mkutano wa baraza la usalama la Kremlin lililo na jukumu la kuhakikisha uwepo wa utulivu katika maeneo 4 ya Ukraine ambayo Putin anadai kuyazingira mwaka jana. Matamshi hayo ya Putin yanakuja siku chache baada ya mlipuko katika mkahawa mmoja huko Saint Petersburg uliosababisha kifo cha mwanablogu anayeunga mkono vita Ukraine.

Hayo yakiarifiwa Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy amefanya ziara nchini Poland ili kutoa shukrani kwa nchi hiyo kwa kusimama na Ukraine tangu kuanza kwa vita hivyo. Zelenskiy ameshikilia kwamba nchi bado inaudhibiti mji wa Bakhmut ambao Kiev inasema wanajeshi wake wamepambana na mashambulizi ya Urusi katika eneo la viwanda la mji huo.