1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Putin: Hatuna dhamira ya kuivamia kijeshi nchi ya NATO

17 Desemba 2023

Rais wa Urusi Vladimir Putin amesema madai ya rais Joe Biden wa Marekani kwamba iwapo Moscow itashinda vita nchini Ukraine itapata ujasiri wa kuishambulia nchi mwanachama wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO hayana msingi.

https://p.dw.com/p/4aGMs
Rais wa Urusi Vladimir Putin
Rais wa Urusi Vladimir PutinPicha: Alexander Zemlianichenko/REUTERS

Putin ameyasema hayo kwenye mahojiano na kituo cha televisheni ya taifa ya Urusi cha Rossiya yaliyorushwa leo Jumapili. 

Kiongozi huyo amesema rais Biden anaufahamu ukweli kwamba Urusi haina dhamira ya kuingia vitani na muungano wa kijeshi wa NATO na kwamba matamshi yake aliyoyatoa mapema mwezi huu ni hayana msingi.

Putin amesema onyo la Biden lilikuwa ni sehemu ya juhudi za utawala mjini Washington kuhalalisha kile amekitaja kuwa "sera zisizo rafiki" za Marekani dhidi ya Urusi.

Kwenye matamshi yake Biden hakutoa ushahidi wowote wa madai yake kuhusu Urusi na dhamira ya Moscow kuivamia nchi yoyote ya NATO.