SiasaAsia
Putin kukutana na Jinping
17 Oktoba 2023Matangazo
China inawaalika wawakilishi wa nchi 130 kuhudhuria mkutano kuhusu mradi mkubwa wa biashara na miundombinu wa Rais Xi.
Ikulu ya Kremlin ilisema Rais Putin angelifanya mazunguzo na Xi kandoni mwa mkutano huo wa Jumatano (Oktoba 18), utakaojikita juu ya masuala ya kimataifa na kikanda.
Soma zaidi: Putin akubali pendekezo la China kwa mzozo wa Ukraine
Siku ya Jumanne (Oktoba 17) Xi aliufungua mkutano wa Beijing kwa kufanya mazungumzo na Rais Gabriel Boric wa Chile na Rais Kassym-Jomart Tokayev wa Kazakhstan.
Baadaye alikutana na Waziri Mkuu wa Hungary Viktor Orban akimueleza kama rafiki na kumshukuru kwa kuunga mkono mradi wa biashara na miundombinu wa China.
Xi pia alikutana na mawaziri wakuu wa Ethiopia na Papua New Guinea.