Pyongyang. Korea kaskazini kuongeza silaha za kinuklia.
22 Machi 2005Korea ya kaskazini imesema kuwa imeongeza silaha zake za kinuklia kuisaidia kujizuwia na shambulio lolote kutoka Marekani. Shirika la habari la Korea ya kusini limesema , likikariri vyombo vya habari vya Korea ya kaskazini.
Taarifa hizo zimekuja wakati waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Bibi Condoleezza Rice amemaliza ziara yake ya wiki moja ya mataifa ya Asia ambapo suala la silaha za kinuklia za Korea ya kaskazini lilichukua uzito wa juu kabisa.
Marekani imesema inaamini kuwa Korea ya kaskazini ina hadi mabomu mawili na madini ya kutosha ya plutonium kwa ajili ya kutengeneza mabomu zaidi ya nuklia. Mwezi mmoja uliopita, Korea ya kaskazini ilitishia kuongeza idadi ya silaha zake za kinuklia na pia ghafla ikajiondoa katika mazungumzo juu ya mpango wake huo wa silaha za kinuklia.