PYONGYANG: Korea kaskazini tishio.
2 Mei 2005Matangazo
Washington na Korea Kusini zimesema kuwa Korea Kaskazini imerusha kombora la masafa mafupi la majaribio katika pwani ya Japan.
Jaribio limetokea wakati ambako hali wasiwasi imetanda huku Pyogyang ikidhaniwa labda inaunda makombora yenye mabomu ya nuklia.
Swala hili nyeti litazungumziwa katika mkutano wa kimataifa leo hii mjini New York utakao zungumzia kwa kina juu ya kusambaa kwa silaha za kinuklia.
Korea Kaskazini imetakiwa kurudi katika mazungumzo ya wanachama sita yenye azma ya kusimamisha mpango wa silaha za kinuklia wa taifa hilo la kikomunisti.
Mazungumzo hayo ya nchi wanachama sita ni pamoja na Korea zote mbili, Japan, Urusi, China na Marekani yalikwama tangu mwaka jana na tarehe mpya ya kuanza tena kwa mashauriano haijatangazwa bado.