1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Qatar yamuachia huru mwanaharakati Mkenya

Josephat Charo
3 Juni 2021

Afisa wa ulinzi raia wa Kenya, Malcolm Bidali aliyeshitakiwa na Qatar kwa kupokea fedha kutoka kwa wakala wa kigeni kueneza taarifa zisizo sahihi katika taifa hilo la Ghuba ameachiwa huru.

https://p.dw.com/p/3uNte
Iran Teheran Straßenszene vor der Präsidentschaftswahl
Picha: Morteza Nikoubazl/NurPhoto/picture alliance

Hayo yamesemwa na mashirika ya kutetea haki za binadamu siku ya Jumatano.

Katika taarifa yake kwenye mtandao wa kijamii wa twitter, shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu Amnesty International lilisema Malcolm hayuko chini ya ulinzi, lakini anakabiliwa na mashitaka yanayoonekana ya kusingiziwa nchini Qatar kuhusiana na uanaharakati wake halali.

Shirika hilo aidha limetaka mashitaka yote kutokana na kazi yake ya kutetea haki za binadamu yafutiliwe mbali.

Shirika lengine la haki za binadamu Migrants Rights pia limethibitisha kuachiwa huru kwa Malcolm, anayefahamika kwa jina la kiuandishi la Noah.