1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Qatar:Mazungumzo ya kusitisha vita Gaza yako hatua za mwisho

14 Januari 2025

Qatar ambayo ndio mpatanishi mkuu katika mazungumzo ya kumaliza vita vya Gaza na kuwachiliwa mateka yamefikia leo hatua za mwisho.Imeongeza kuwa ina matumaini makubaliano huenda yakafikiwa hivi karibuni.

https://p.dw.com/p/4p8iG

Msemaji wa Wizara ya mambo ya nje ya Qatar Majed al-Ansari ameuambia mkutano wa waandishi habari kuwa wajumbe wamefikia sehemu ambapo masuala muhimu yaliyokuwa yakizuia muafaka kupatikana yameshughulikiwa.

"Ni muhimu sana kuzingatia tusiwape watu matarajio ambayo siyo sawa na kile kinachotokea sasa hivi. Tunaamini kuwa tumepiga hatua kubwa," alisema Majed.

"Tunaamini pia tuko katika hatua za mwisho. Lakini ni wazi kwamba makubaliano hayawezi kuwa makubaliano hadi litakapotolewa tangazo rasmi kuwa yamefikiwa," aliongeza.

Mapacha vichanga wauwawa Gaza

Soma pia: Makubaliano ya kusitisha vita vya Gaza yanukia

"Kwa hivyo tusisherehekee kupita kiasi kwa kinachotokea sasa. Tuwe na Subira, Lakini bila shaka tunayo tamaa.”

Hapo jana, Rais wa Marekani anayeondoka Joe Biden alisema mpango huo unakaribia kukamilishwa, ikiwa ni siku chache tu kabla ya kuapishwa kwa mrithi wake, Donald Trump.

Misri, Qatar na Marekani zimeimarisha juhudi za kufikiwa mpango wa usitishwaji vita ili kuwezesha kuwachiwa huru kwa mateka wanaoshikiliwa Gaza tangu shambulizi la Hamas la Oktoba 7, 2023 kusini mwa Israel.