1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

RABAT: Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani, Frank -Walter Steinmeier yuko kaskazini mwa bara la Afrika

18 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCrj

Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani, Frank- Walter Steinmeier, ambae sasa yuko nchini Morocco, ameipongeza serikali ya Morocco kwa juhudi zinazofanywa na tume ya ukweli juu ya mateso na vitendo vingine vya dhuluma vilivyopitishiwa wapinzani miaka ya 60 na 70 wakati wa utawala wa mfalme Hassan wa II. Tume hiyo ilianza uchunguzi miaka miwili iliopita chini ya utawala wa mtoto wa mfalme huyo Mohammed wa VI.

Akiwa nchini Tunisia, Steinmeier alizungumzia juu ya swala la wahamiaji haramu wanaotafuta kuingia Ulaya na kwamba mkutano kati nya nchi za Ulaya na eneo la Maghreb kaskazini mwa Afrika uliopangwa kufanyika mjini Tripoli nchini Libya wiki ijayo utaweza kusaidia katika ustawi wa eneo hilo. Steinmeier ataelekea nchini Mauritania baadae hii leo, ikiwa ni hatua ya mwisho ya ziara yake ndefu katika nchi za Afrika ya kaskazini.