RABAT:Zaidi ya wafungwa 400 wa kimoroko Sahara Magharibi waachiliwa huru
19 Agosti 2005Zaidi ya wafungwa wa kivita 400 wa Kimoroko waliokuwa wanashikiliwa na wapiganaji wa chini kwa chini wa Sahara Magharibi kwa miaka 20,sasa wamerejea makwao.
Shirika la kimataifa la msalaba mwekundu lilisema wafungwa wote wa kivita waliokuwa wanashikiliwa na chama cha POLISARIO kinachoungwa mkono na Algeria sasa wameachwa huru. Wao walikuwa wafungwa wa kivita walioshikiliwa kwa muda mrefu kabisa duniani.
Sahara Magharibi ili na utajiri mkubwa wa madini ni eneo ambalo liko kwenye mzozo tangu Uhispania iondoke huko mwaka 1975 .
Nchi jirani ya Moroko iliivamia Sahara Magharibi ikidai eneo hilo ni sehemu ya ardhi yake.
Baadae chama cha POLISARIO kIkajitangazia jamhuri ya sahara na kikaanzisha vita vya chini kwa chini. Marekani iliingilia kati ili wafungwa hao waachwe huru.