1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMamlaka ya Palestina

Wapalestina watafuta makao baada ya amri ya kuondoka Gaza

3 Julai 2024

Wapalestina wanaendelea kutafuta makao baada ya kukimbia makaazi yao kusini mwa Gaza na kulalamikia uhaba wa maji wakati ambapo Israel inaendelea na mashambulizi ya kijeshi katika eneo hilo lililo na idadi kubwa ya watu.

https://p.dw.com/p/4hoxY
Mapigano katika ukanda wa Gaza | Khan Younis
Wapalestina wameanza kuhama baada ya jeshi la Israel kuwamuru kuondoka mara moja kabla ya kutokea mashambulizi mapya ya ardhini huko Khan Yunis.Picha: Ali Jadallah/Anadolu/picture alliance

Kulingana na wakaazi, vikosi vya Israel vimefanya mashambulizi mapya katika mji wa kusini wa Rafah wakati ambapo kumeshuhudiwa mapigano makali na wanamgambo wa Kipalestina usiku wa kuamkia leo.

Soma pia: Wanamgambo wa Kipalestina wavurumisha makombora Israel

Maafisa wa afya wanasema karibu watu 12 wameuwawa katika mashambulizi mapya katika eneo la kati na kaskazini mwa Gaza.

Viongozi wa Israel wamesema wanamalizia awamu ya mapigano makali na wanamgambo wa Hamas na baada ya hapo watagaeukia operesheni yenye malengo katika vita hivyo.