1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mbaroni kwa kupanga mashambulizi dhidi ya ubalozi wa Israel

Angela Mdungu
20 Oktoba 2024

Polisi nchini Ujerumani imemkamata raia mmoja wa Libya kwa tuhuma za kuhusika na kundi linalojiita dola la Kiislamu na kwa kupanga mashambulizi dhidi ya ubalozi wa Israel mjini Berlin.

https://p.dw.com/p/4lzxx
Polisi wa Ujerumani akifanya ukaguzi katika kutimiza majukumu yake.
Polisi Ujerumani wamemkamata raia wa Libya kwa kupanga njama kuushambulia ubalozi wa Israel mjin BerlinPicha: Revierfoto/Revierfoto

Kulingana na gazeti la kila siku la Bild, kikosi maalumu cha polisi kilivamia makazi ya kijana huyo mwenye miaka 28 siku ya Jumamosi nje kidogo mwa mji mkuu Berlin na kumtia nguvuni.

Soma zaidiPolisi mjini Munich wamuua mshukiwa wa 'ugaidi' karibu na ubalozi wa Israel

Gazeti hilo limeeleza kuwa polisi walichukua hatua hiyo baada ya kupewa taarifa na shirika la kijasusi la nchi nyingine na kuwa mtuhumiwa hakuwa katika orodha ya kundi lolole linalofuatiliwa na polisi nchini Ujerumani.

Kijana huyo anadhaniwa kuwa aliingia Ujerumani Novemba mwaka 2022 na kuomba hifadhi mwezi Januari mwaka uliofuata, ombi ambalo hata hivyo lilikataliwa Septemba 2023.