Uchaguzi mkuu wa Uhispania unafanyika leo
23 Julai 2023Matangazo
Waziri Mkuu Pedro Sanchez aliitisha uchaguzi wa mapema, baada ya chama chake cha Kisosholisti na mshirika wake chama cha Unidas Podemos, kuanguka katika uchaguzi wa serikali za mitaa mnamo mwezi Mei. Sanchez amekuwa Waziri Mkuu wa Uhispania tangu mwaka 2018.
Soma zaidi: Uhispania yafanya uchaguzi muhimu wa serikali za mitaa
Utafiti mwingi wa kura za maoni kuhusu uchaguzi wa leo unakiweka chama cha Kihafidhina cha People's Party ambacho kilishinda uchaguzi wa Mei, mbele ya Wasosholisti, lakini kitahitaji uungwaji mkono wa chama chenye mrengo mkali wa kulia cha Vox Party ikiwa watatakiwa kuunda serikali mpya.