Raia wa Uzbekistan wapiga kura kurefusha utawala wa rais
9 Julai 2023Raia wa Uzbekistan wamepiga kura leo Jumapili katika uchaguzi wa rais ambapo Rais Shavkat Mirziyoyev anawania kurefusha utawala wake kwa muhula mwinginé wa mika saba. Uchaguzi huo umefanyika ikiwa ni miezi kadhaa baada ya rais huyo kubadili Katiba ili kuongeza ukomo wa utawala, ambapo kabla ulitakiwa kukamilika mwaka 2026.
Awali, Mirzi-yoyev aliendesha kura ya maoni mnamo mwezi Aprili ya marekebisho ya katiba ambayo iliongeza mihula ya urais kutoka miaka mitano hadi miaka saba. Hata hivyo bado hakuna vyama vya upinzani vyenye nguvu au wanasiasa wanaotarajiwa kuleta ushindani kwa kiongozi hiyo katika uchaguzi wa Jumapili.Uzbekistan yaahidi kuisaidia Marekani kuchunguza ugaidi
Kama mataifa mengine ya Asia ya kati, Uzbekistan inajaribu kupunguza athari za vikwazo vya nchi za Magharibi vilivyowekwa dhidi ya mshirika wake wa jadi wa kibiashara Urusi, kufuatia vita vya Ukraine.