SiasaMali
Raia wayakimbia makaazi yao kaskazini mwa Mali
25 Novemba 2022Matangazo
Wanamgambo wa Dola la Kiislamu katika eneo zima la Sahara walishambulia maeneo ya Gao na Menaka mnamo mwezi Machi na kusababisha mapigano makubwa na makundi yaliyojihami na makundi hasimu ya kijihadi.
Mashuhuda na duru zengine zilizozungumza na shirika la habari la Ufaransa, AFP, wamesema wapiganaji hao wa kijihadi walipewa shinikizo katika maeneo hayo na wanaharakati wa haki za binadamu wanasema watu wameuwawa.
Miji ya kimkakati ya Gao na Menaka kwa muda mrefu sasa imekuwa ikisumbuliwa sana na mashambulizi haya ya kijihadi ambayo yamedumu kwa mwongo mmoja sasa nchini Mali.