Raila ashinikiza "haki" kabla ya mazungumzo Kenya
21 Julai 2024Matangazo
Raila, ameyasema hayo kufuatia wiki za maandamano ya kupinga nyongeza ya kodi, sera ambayo Rais William Rutoaliiondoa baada ya maandamano ya amani kusababisha ghasia na makumi ya watu kuuawa baada ya baadhi ya waandamanaji kuvamia bunge.
Soma pia: Jeshi la polisi Kenya lapiga marufuku maandamano Nairobi
Raila ambaye alishindwa na Ruto katika uchaguzi wa urais wa 2022, amesema lazima kuwe na "mazungumzo ya kitaifa" kati ya makundi tofauti ya jamii.
Kupitia mtandao wa kijamii wa X, Raila ameandika kwamba mazungumzo kama hayo yanapaswa kuyajumuisha makundi mbalimbali ikiwa ni pamoja na vijana, serikali, viongozi wa dini, wataalamu wa afya, wanasheria na walimu.