1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMamlaka ya Palestina

Kiongozi wa Palestina amteua Waziri Mkuu mpya

15 Machi 2024

Rais wa mamlaka ya ndani ya Wapalestina, Mahmoud Abbas amemteua mshauri wake wa muda mrefu wa masuala ya uchumi kuwa waziri mkuu mpya wa mamlaka hiyo, shirika rasmi la habari la Palestina, WAFA limearifu.

https://p.dw.com/p/4dXMM
Rais Mahmoud Abbas amteua mchumi kuwa waziri mkuu mpya
Rais wa Palestina Mahmud Abbas akiwa kwenye mkutano wa dharura wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu na Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC), mjini Riyadh, Saudi Arabia, Novemba 11, 2023.Picha: Saudi Press Agency/Newscom/picture alliance

Mustafa anateuliwa wiki mbili baada ya aliyekuwa Waziri Mkuu Mohammad Shtayyeh kujiuzulu na serikali yake akiangazia mabadiliko katika Ukanda wa Gaza. 

Mwanauchumi huyo ambaye ni mjumbe wa tume huru tendaji ya Chama cha Ukombozi wa Wapalestina PLO, amewahi pia kuwa naibu waziri wa masuala ya uchumi na mjumbe wa Wakfu wa Uwekezaji wa Palestina.

Mwanasiasa huyo, 69 sasa anakabiliwa na jukumu la kuunda serikali mpya ya Mamlaka ya Palestina, yenye ushawishi hafifu katika maeneo ya Ukingo wa Magharibi unaokaliwa na Israel.

Tangu mwaka 2007, kumekuwa na mgawanyiko wa udhibiti wa maeneo ya Palestina. Wakati Ukingo wa Magharibi ukitawaliwa na serikali ya Abbas, Gaza iko chini ya kundi la Hamas.