1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaNiger

Rais aliyepinduliwa Niger atembelewa na daktari

12 Agosti 2023

Rais aliyepinduliwa nchini Niger Mohammed Bazoum leo ameonana na daktari siku moja baada ya Jumuiya ya Kimataifa kuelezea wasiwasi mkubwa juu ya hali ya afya ya kiongozi huyo aliye kizuizini.

https://p.dw.com/p/4V6AT
Frankreich Paris | demonstration für Präsident Mohamed Bazoum vor der Botschaft des Niger
Picha: Sophie Garcia/AP Photo/picture alliance

Hayo yameripotiwa jioni hii na shirika la habari la AFP likinukuu duru za watu walio karibu na kiongozi huyo. Chanzo hicho kimesema Bazoum ametembelewa na daktari ambaye pia amepeleka chakula kwa ajili ya yake, mkewe na mtoto wao wa kiume ambao kwa pamoja wanashikiliwa.

Hapo jana Umoja wa Ulaya na Umoja wa Afrika zilijiunga na Marekani na nchi nyingine duniani kutoa tahadhari juu ya hali ya afya kiongozi huyo anayeshikiliwa kwa zaidi ya wiki mbili tangu majenerali walipompindua.

Hayo yanajiri wakati watawala wa kijeshi bado wamepuuza miito ya kikanda na kimataifa ya kuachia madaraka na kumrejesha Bazoum madarakani, licha ya kitisho cha uingiliaji kati kijeshi.