1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Biden aahidi usaidizi kwa waathiriwa wa moto, Maui

22 Agosti 2023

Rais wa Marekani Joe Biden amekitembeela kisiwa cha Maui kilichoteketea kwa moto wa nyika kiasi wiki mbili zilizopita na kuahidi kuwa serikali yake itawasaidia waathirika wa mkasa huo bila ukomo.

https://p.dw.com/p/4VQUC
Rais wa Marekani Joe Biden na mkewe Jill Biden
Rais wa Marekani Joe Biden na mkewe Jill BidenPicha: Evan Vucci/AP/picture alliance

Biden na mkewe Jill walisafiri kwenda kwenye kisiwa hicho cha jimbo la Hawaii kutoa mkono wa pole kwa familia za watu 114 walipoteza maisha pamoja na manusura wa mkasa huo wa moto unaotajwa kubwa ndiyo mbaya zaidi nchini Marekani katika muda wa karne nzima.

Akizungumza chini ya mti mkubwa ulioungua moto rais Biden amesema taifa linaomboleza pamoja na watu wa kisiwa cha Maui na serikali mjini Washington haitawatupa mkono.

Kabla ya kutoa hotuba hiyo Biden alizunguka kwa helikopta kujionea uharibifu ulitokana na janga la moto hususani kwenye mji wa kihistoria wa Lahaina ambao karibu kila kitu kiliteketea.