1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Biden kuzungumza na Ruto wa Kenya Alhamis

21 Mei 2024

Rais wa Marekani Joe Biden atamkaribisha Alhamisi wiki hii rais wa Kenya William Ruto kwa mazungumzo mapana yanayotarajiwa kujumuisha kufutwa kwa deni la Kenya pamoja.

https://p.dw.com/p/4g6Bd
Kenia/USA Kenias Präsident William Ruto legt einen Kranz an den Gräbern von Martin Luther King Jr. und Corett Scott King
Picha: John Bazemore/ASSOCIATED PRESS/picture alliance

Mengine yaliyoko kwenye ajenda pia ni hatua zinazotakiwa kufuata kuzisaidia Haiti, Ukraine, Sudan na maeneo mengine ya mizozo.

Kenya imekuwa ikikabiliana na changamoto kubwa ya fedha na afisa wa cheo cha juu serikalini ameliambia shirika la habari la Reuters Jumatatu kwamba Marekani inazihimiza nchi zilizotoa mikopo mikubwa kama vile China, ambayo ni mkopeshaji mkubwa wa Kenya, ziyafutie baadhi ya madeni mataifa yaliyolemewa na mizigo ya madeni.

Marekani pia inazihimiza taasisi za kimataifa za fedha ziipe Kenya na nchi nyingine mikopo yenye riba nafuu.

Biden na Ruto pia watazungumzia ushirikiano wa kiusalama huku mahusiano kati ya Marekani na Kenya yakitanuka kutoka kuwa ya kikanda hadi ushirikiano wa kimataifa.

Biden na Ruto wanatarajiwa kufanya mkutano wa pamoja na waandishi habari baada ya mazungumzo yao na baadaye kuhudhuria dhifa ya kitaifa.