1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Duterte asema Mungu amesema naye

28 Oktoba 2016

Rais Rodrigo Duterte wa Ufilipino, ambaye mara kadhaa ametumia lugha zisizofaa kuwatusi baadhi ya viongozi duniani anasema ameacha kufanya hivyo, baada ya kile ambayo anadai kuwa amesikia sauti ya Mungu.

https://p.dw.com/p/2RqLM
Phillippinen Rodrigo Duterte
Picha: Reuters/L. Daval Jr

Rais Durerte amewahi kumtusi kiongozi wa kanisa katoliki dunia Baba mtakatifu Fransis kwa kumuita mtoto wa kahaba, pia amewahi kumtusi Rais wa Marekani Barak Obama kwa kumwambia aende jehanamu.

Matumizi ya lugha za matusi na za kuudhi imekuwa ni utambulisho wake hasa pale; anapotishia kuua watu ambao wamekuwa wakijihusisha na biashara ya dawa za kulevya; hii ikiwa ni sehemu ya juhudi zake katika kupambana na matumizi ya dawa za kulevya ambazo zimeua maelfu ya watu tangu aingine madarakani mwishoni mwa mwezi Juni.

Ametoa kauli hiyo wakati akiwasili katika eneo la kusini mwa mji wa Davao jion ya alhamis, akitokea nchini Japan, anasema alipokuwa akisafiri kurudi nyumbani alikuwa anaangalia angani wakati kila mtu akiwa amelala na wengine wakikoroma na mara akasikia sauti ikisema " kama hutaacha kutukana nitaishusha hii ndege chini sasa hivi alisema Duterte.

Kwa hiyo nimemuahidi Mungu sitaendelea tena kutumia maneno yasiyofaa, kuapa na kila kitu kwa hiyo mnisikie vizuri mara zote kwa sababu ahadi kwa Mungu ni ahadi kwa watu wa Ufilipino,ahadi hiyo imeshangiliwa kwa makofi na akaonya kuwa wasipige makofi sana ama sivyo maana halisi inaweza kupotea.

USA Washington Besuch Papst Franziskus mit Obama
Baba Mtakatifu Fransis akiwa na Rais ObamaPicha: Getty Images/AFP/V. Pinto

Mwaka jana aliwashangaza waumini wa kanisa katoliki nchini Ufilipino ambao ni wengi zaidi nchini humo, alipoelezea kuwa amekerwa sana na msongamano wa magari, ambao umemkwamisha barabarani kwa muda wakati baba mtakatifu Fransis alipotembelea mji mkuu wa nchi hiyo Manila, aliwambia mkusanyiko wa wafuasi wake kuwa alitaka kumpigia simu Papa na kumwambia "wewe mwana wa kahaba rudi nyumbani kwenu na usitembelee tena mahali hapa", japo baadae aliomba radhi baada ya maaskofu wa kanisa hilo kuelezea kushtushwa na kauli hiyo.

Hakuna uhakika bado, kama rais huyo ambaye pia amekuwa akifananishwa na mgombea Urais wa Marekani kwa chama cha Republican Donald Trump, ambaye pia amekuwa akitumia lugha zisizofaa, kama atatekeleza ahadi yake. Duterte amewahi kutoa kauli kama hiyo mwezi Juni, mara alipokuwa imethibitishwa kuwa ameshinda uchaguzi wa rais uliofanyika Me 9.

Mwandishi: Celina Mwakabwale/AP

Mhariri: Mohammed Khelef